Polisi kwenye mji wa Lagos nchini Nigeria wanasema kuwa wamevunja ubalozi bandia ambapo matapeli raia wa China na Nigeria, wamekuwa wakiwaibia watu maelfu ya dolla kwa kuwapa visa bandia na kuwaahidi kuwa watafanya kazi katika nchi za Caribbean.
Kufuatia oparesheni kubwa, polisi waliwakamata raia wawili wa China na wengine wawili raia wa Nigeria wa ubalozi huo bandia katika vitongoji vya mji wa Lagos.
Wale walitapeliwa wanasema kuwa walilipa hadi dola 4000 kila mmoja kwa tikiti na visa ilin kusafiri kwenda Trinidad na Tobago, baada ya kuhaidiwa ajira zenye malipo mazuri wanapofika.
Lakini wale waliowasili wakiwa na stakabadhi hizo bandia walikamatwa uwanja wa ndege ya kurudishwa Nigeria.
"Walinipiga na kuninyima chakula kwa siku mbili, nina bahati walinirudisha nyumbani," mmoja wa waathiriwa alisema.
Ubalozi wa Trinidad na Tobago ulisema kwa hauna maajenti ya kutoa visa wala uhusiano na washukiwa wa kichina waliokamatwa.
0 on: " Ubalozi bandia wa Tridad na Tobago wavunjwa Nigeria "