visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Tuesday, December 13, 2016

Katibu MKuu mpya wa Umoja wa Mataifa Guterres aapishwa

Katibu MKuu mpya wa Umoja wa Mataifa Guterres aapishwa,

Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres, ameapishwa kuwa Katibu MKuu mpya wa Umoja wa Mataifa, kuja kurithi mikoba ya Ban Ki-moon


Guterres alikula kiapo jana Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, mbele ya Rais wa Baraza Kuu la umoja huo, Peter Thomson. Guterres atashika rasmi hatamu za kuiongoza taasisi kubwa zaidi duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe Mosi Januari mwakani. Katibu Mkuu wa sasa wa umoja huo, Ban Ki-moon atakamilisha kipindi chake cha pili tarehe 31 Disemba.

Mara baada ya kuapishwa, Antonio Gutteres, ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema: "Woga umewasukuma watu wa matabaka mbali mbali kuchukua maamuzi fulani, na lazima tuelewe mahitaji yao na kutimiza matakwa yao, bila kupoteza dira ya thamani zetu za kiutu na kiulimwengu." Ameongeza kuwa, wakati umefika wa kuangalia upya uhusiano kati ya viongozi na wananchi na kusisitizia udharura wa watawala kuvisikiliza vilio vya wanaowatawala.
Kadhalika ametahadharisha kuhusu siasa na sera alizosema ni hatari za kuwahadaa watu na kuongeza kuwa, zimeshamiri na kuenea sana duniani.

Aidha raia huyo wa Ureno ameutaka Umoja wa Mataifa utambue na kukubali changamoto zinazoukabili na kuzitafutia ufumbuzi.


0 on: " Katibu MKuu mpya wa Umoja wa Mataifa Guterres aapishwa "