visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Thursday, December 15, 2016

Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania

Maxence Melo
Maxence Melo
Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums Maxence Melo anashikiliwa na polisi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamii Forums Melo anashikiliwa kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Alitarijiwa kufikishwa mahakamani Jumatano asubuhi lakini wakili wake ameambia BBC hilo halikufanyika.
Badala yake, taarifa zinadokeza huenda akafikishwa kortini Jumanne asubuhi.
Wakili wa Bw Melo anatafakari uwezekano wa kuwasilisha ombi kortini kupinga kuzuiliwa kwa mteja wake kwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa kortini.

0 on: " Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania "