visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Monday, December 5, 2016

Algeria yarudisha makwao Wahamiaji wa Afrika magharibi

Algeria yarudisha makwao Wahamiaji wa Afrika magharibi
Wanaharakati wa Haki za Binadamu wanasema Mamlaka nchini Algeria zimeanza kutekeleza mipango ya kuwaondoa maelfu ya Wahamiaji kutoka Afrika Magharibi.
Wamesema polisi wa kuzuia ghasia wamewakamata wanawake, wanaume na watoto katika siku za hivi karibuni na kuwashikilia katika kambi iliyoko karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Algiers, kwenye pwani ya Mediterranean.
Habari zinasema mabasi 11 yameanza safari yakiwa na mamia ya Wahamiaji hao, kuelekea mji wa kusini wa Tamanrasset ukingoni mwa jangwa la Sahara.
Serikali ya Algeria haijasema chochote kuhusu nini kinachofuata kuhusu Wahamiaji hao, lakini kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC katika eneo hilo, inaonekana kama watarudishwa katika nchi walizotoka.
Septemba mwaka huu serikali ya nchi hiyo ilitangaza mipango ya kuwaondoa wahamiaji hao kutoka Afrika magharibi, ambao ni wengi.

0 on: " Algeria yarudisha makwao Wahamiaji wa Afrika magharibi "