visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Saturday, December 17, 2016

Oscar kuzidi Messi na Ronaldo kwa kulipwa pesa nyingi

Mchezaji wa Chelsea Oscar anatarajiwa kuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani atakapohamia Ligi Kuu ya Uchina mwezi Januari.
Shanghai SIPG wanatarajiwa kulipa £60m kumchukua kiungo huyo wa kati kutoka Brazil.
Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar, 25, ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai.
Taarifa zinasema atakuwa analipwa £400,000 kila wiki (£20.8m kila mwaka), ingawa huenda akapitwa haraka kwani kuna taarifa kwamba klabu za China zinajiandaa kulipa pesa nyingi kununua wachezaji wengine Januari. Mshahara wa Oscar ni sawa na £57,143 kila siku, au £2,381 kwa saa, au £39 kila dakika.
Kuna taarifa huenda Shanghai Shenhua ,ambao mkufunzi wao kwa sasa ni Gus Poyet aliyetoka Sunderland, wanapanga kumnunua nyota wa zamani wa Manchester United na Manchester City Carlos Tevez kutoka Boca Juniors. Tevez atakuwa analipwa £31.5m kila mwaka, sawa na £605,000 kila wiki.
France Football wanasema mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavaninaye huenda akahamia Tianjin Quanjian, walio chini ya beki wa zamani wa Italia Fabio Cannavaro, kwa euro 50m (£41.79m) fambapo atakuwa akilipwa £16.7m kila mwaka.
Mwenzake kwenye klabu Javier Pastore kutoka Argentina pia huenda akahamia China.
Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez pia amehushishwa na kuhamia Hebei China Fortune, ambayo mkufunzi wake kwa sasa ni aliyekuwa meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini. Sanchez, anatarajiwa kulipwa £500,000 kila wiki iwapo atakubali kuhama.






Klabu ambazo zimetumia pesa nyingi zaidi karibuni nchini China ni Shanghai SIPG, Jiangsu Suning, mabingwa wa ligi Guangzhou Evergrande Taobao na Shanghai Shenhua.
Chanzo BBC Swahili


0 on: " Oscar kuzidi Messi na Ronaldo kwa kulipwa pesa nyingi "