Bao la kichwa la Ashley Williams dakika ya 86 liliiwezesha Everton kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal.
Ushindi wa Everton umeizuia Arsenal kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Uingereza na kudhoofisha matumaini ya ubingwa.
Matokeo hayo pia yanaifanya Chelsea ijitanue kileleni kwa tofauti ya pointi sita baada ya kuwafunga wachovu Sunderland goli 1 -0 Goli la chelsea lilifungwa na Cesc Fabregas
Arsenal ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Alexis Sanchez na kutoa dalili za ushindi mwingine kwa Arsenal.
Sanchez alifunga kwa njia ya mkwaju wa adhabu ndogo ulioguswa kidogo na kumpoteza kipa wa Everton dakika ya 20.
Everton walifanikiwa kusawazisha dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia kwa Seamus Coleman
Wakati muda ukiyoyoma, Williams alifunga kwa kichwa kufuatia kona iliyochongwa na Ross Barkley kuipa Everton ushindi wake wa kwanza nyumbani tangu Oktoba.
0 on: " Arsenal yaangukia pua EPL, ni baada ya kufungwa na Everton "