Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla, atafanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, ambao utamfanya kusalia nje ya mchezo kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Uhispania, hajashiriki mechi yoyote tangu katikati mwa mwezi Oktoba kutokana na jeraha hilo alilolipata walipokuwa wakikabiliana na Ludogorets katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Katika mechi hiyo Arsenal walitoka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Ludogorets.
Arsenal wamesema shida yake ''bado haijabadilika'' na atasafiri kuelekea Sweden wiki ijayo kwa upasuaji.
Cazorla, alikosa mechi saba msimu uliopita kutokana na jeraha la goti.
Amefunga magoli mawili katika mechi 11 zote alizoshiriki na klabu hiyo ya Gunners msimu huu.
Arsenal imesema,''upasuaji unahitajika kwa kifundo chake cha mguu wa kulia.''
0 on: " Santi Cazorla kukaa nje kwa miezi mitatu "