Mchezaji wa klabu Mbao FC U20 Ismail amefariki dunia akiwa uwanjani katika Ligi kuu ya vijana wasio zidi miaka ishirini (U20) dhidi ya Mwadui FC.
Ismail alianza mechi salama na alibahatika kuifungia klabu yake bao moja katika dakika 25' lakini ghafla dakika la 75' akiwa pekee yake alianguka ghafla na kufariki.
Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na juhudi kubwa zilifanyika kuokoa maisha ya kinda huyo, lakini haikuwezekana.
“Inaonekana alishafariki dunia pale uwanjani, tulifanya juhudi kubwa mimi na wenzangu. Tulisaidiana na watu wengine pia waliokuwa uwanjani, lakini ilionekana hakukuwa na majibu mazuri,” alisema mmoja wa madaktari waliojaribu kuokoa maisha ya kijana huyo.
Tuwakumbushe kuwa Ismail ndie mfungaji bora wa Ligii na tayari klabu yake ilimuhaidi kuwa akimaliza msimu huu atajiunga na Mbao FC ya daraja ya kwanza msimu ujao.
Msiba huu umetonesha msiba wa Taifa la Tanzania, Afrika na familia ya wapenda soka duniani huku kifo cha kijana inaleta kumbukumbu la kifo cha Marc Vivien Foe mwaka 2003 ambaye naye alifariki uwanjani ghafla
0 on: " Mchezaji wa Mbao FC U 20 (Tanzania), Ismail Mrisho afariki uwanjani "