Mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio hilo alikamatwa na kupelekwa kwenye makao makuu ya polisi,kisha kwenye makao makuu ya Idara ya ujasusi kwa kusikilizwa, kwa mujibu wa serikali ya Chad.
Mtu, raia wa Chad, alikuwa amepanda kwenye pikipiki wakati alifyatua risasi akielekeza kwenye ubalozi wa Marekani, mita mia moja kutoka Ikulu ya rais wa Chad.
Katika waraka aliyokutwa nao, mtuhumiwa huyo aikua alijiunga na kundi la Islamic State, chanzo kilio karibu na uchunguzi kimebaini.
Kwa mujibu wa polisi, silaha iliyotumiwa ni bastola iliyotengenezwa nchini Uturuki.
Ubalozi wa Marekani ulikuwa ulizingirwa na vikosi vya usalama baada ya tukio hilo.
Itakumbukwa kwamba mwezi Juni 2015, makao makuu ya polisi na chuo cha polisi katika mji muu wa Chad vilishambuliwa, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya ishirini na zaidi ya 100 kujeruhiwa.
0 on: " Milio ya risasi yasikika kwenye ubalozi wa Marekani nchini Chad "