Mwanamke ambaye picha yake imekuwa ikiongezwa maneno na ujumbe wa utani na kusambazwa mtandaoni kwa sababu ya muonekano wake, amewashambulia wanaotumia picha hizo na kumcheka.
Lizzie Velasquez, 27 anayetoka Austin, Texas hutoa mihadhara ya kuwahamasisha watu na amewahi kutoa hotuba katika kipindi cha TED.
Aidha, ana wafuasi wengi sana mtandaoni.
Alizaliwa na tatizo nadra sana la kiafya ambalo huufanya mwili wake kushindwa kuhifadhi mafuta.
"Naandika ujumbe huu sio kama mwathiriwa lakini kama mtu anayetumia sauti yake.
- Mwanamke anayedaiwa kuwa na 'sura mbaya' atoa filamu
- Wajua picha hii iliyovuma sana mtandaoni ilitoka wapi?
"Haijalishi muonekano wetu au kimo chetu, unene au wembamba wetu, mwisho wa yote, sisi ni binadamu," aliandika kwenye Instagram.
Kando na picha za Lizzie, wanaosambaza ujumbe wa mzaha mtandaoni ukiwa kwenye picha, ambazo hufahamika kwa Kiingereza kama 'meme', wamekuwa pia wakitumia picha za wanawake wanene, wazee au watu wenye ulemavu.
"Nawaomba mzingatie hilo wakati mwingine mnapotazama picha kama hizi zikisambazwa sana mtandaoni za mtu ambaye hamumfahamu," alisema.
"Wakati huo, huenda ukadhani ni jambo la kuchekesha lakini kwa binadamu aliyewekwa kwenye picha hiyo, labda hisia alizo nazo ni kinyume kabisa."
Chanzo BBC Swahili
0 on: " Mwanamke aliyeshambuliwa mtandaoni ajitetea "