visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Monday, December 5, 2016

Jeshi la Nigeria lasisitiza kung'olewa mizizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram


Mkuu wa jeshi la anga la Nigeria ametoa wito wa kuweko ushirikiano wa vikosi vyote vya majeshi ya nchi hiyo ili kung'oa mizizi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

Sadique Abubakar ameashiria kuongezeka operesheni za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram na kusisitiza udharura wa kuweko uratibu baina ya vikosi vya jeshi na vya ulinzi kwa ajili ya kupatikana matunda mazuri ya mashambulio dhidi ya wanamgambo hao.
Mkuu wa kikosi cha anga cha jeshi la Nigeria ametangaza kuwa, kuna ndege na helikopta za kivita ambazo nchi hiyo itazipokea kutoka kwa Russia na Pakistan ambazo zitatumika katika kukabiliana na hujuma za kigaidi na za wanamgambo.

Aidha Sadique Abubakar amebainisha kwamba, kwa sasa kuna askari zaidi ya 700 wa Nigeria wanaopata mafunzo ya kijeshi katika nchi za Pakistan, China, Uingereza, Afrika Kusini, Misri, Russia na Marekani.
Wakati huo huo, Luteni Jenerali Tukur Buratai, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Nigeria amesema kuwa, analikumbusha jeshi la nchi hiyo kuamiliana na magaidi waliotiwa mbaroni kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Aidha mkuu huyo wa majeshi ya Nigeria amewataka makamanda wote wa jeshi kufanya juhudi za kuwaokoa watu wote waliotekwa nyara na wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
Kutokuwa na uwezo serikali ya Nigeria wa kukabiliana na kundi la Boko Haram kumesababisha vifo vya maelfu ya raia hususan katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.


0 on: " Jeshi la Nigeria lasisitiza kung'olewa mizizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram "