Majivu ya aliyekuwa rais wa Cuba Fidel Castro yamezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.
Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti.
- Mwili wa Fidel Castro kuchomwa
- Wananchi wa Cuba waomboleza
- Fidel Castro afariki dunia akiwa na miaka 90
Hapo jana, rais wa Cuba, Raul Castro, amesema serikali yake itakataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.
Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.
0 on: " Majivu ya mwili wa Fidel Castro yazikwa Santiago, Cuba "