Hatimaye wanajeshi wa Syria wakishirikiana na wanamapambano wa kujitolea wameukomboa kikamilifu mji wa Aleppo (Halab)
Usiku wa kumakia leo, wakazi wa mji huo wametoka mabarabarani kusherehekea ushindi huo kwa shangwe, vifijo na vigelegele, baada ya kupokea habari za kukombolewa kikamilifu mji huo, uliokua moja ya ngome za wanachama wa magenge ya kigaidi nchini humo.
Leteni Jenerali Zaid al-Saleh, Mkurugenzi wa Kamati ya Usalama wa Taifa katika mji wa Aleppo amesema kuwa, asilimia 99 ya maeneo ya mji huo yaliyokuwa yakidhibitiwa na makundi ya kigaidi yamekombolewa na kubainisha kwamba, magaidi waliokuwa katika mji huo ima wameangamizwa au wamejisalimisha kwa vyombo vya usalama.
![]() |
Wananchi wa Syria wakisherehekea kukombolewa Aleppo |
Wakati huo huo, Rami Abdulrahman, Mkurugenzi wa Syrian Observatory for Human Rights amethibitisha habari za kukombolewa kikamilifu mji huo na kwamba magaidi wameondoka katika vijiji sita vya mwisho ambapo walikuwa wamejificha.
Hivi karibuni Rais Bashar al-Assad wa Syria alisema kuukomboa mji wa Aleppo, itakuwa ni hatua kubwa ya kuelekea kumaliza vita na harakati za kigaidi katika nchi hiyo na kwamba litakuwa pigo kwa magenge ya kigaidi na waungaji mkono wao kieneo na kimataifa.
Naye Ibrahim Amin as Sayyid, Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon siku chache zilizopita alisema kuwa, ushindi uliopatikana mjini Aleppo, umetokana na baraka za mujahidina na damu za mashahidi wa muqawama wa Kiislamu na uongozi wao wa kijeshi na kiusalama.
Aleppo au Halab imekuwa miongoni mwa ngome kuu za makundi ya kigaidi nchini Syria kwa kipindi cha zaidi ya miaka 5 sasa.
0 on: " Hatimaye mji wa Aleppo nchini Syria wakombolewa "