![]() |
James Mattis |
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara tangu kushinda urais ambapo amemtangaza jenerali mstaafu James Mattis kama waziri mpya wa ulinzi.
Jenerali Mattis maarufu kama 'Mad Dog', ni mwanajeshi wa zamani aliye na sifa ya kuweka mikakati, kuwa na msimamo mkali na mpinzani mkubwa wa Iran.
Trump alimfananisha James Mattis na Jenerali George Patton, kamanda wa jeshi la Marekani kwenye vita vikuu vya pili ambapo wenzake walimpa jina la '' Old Blood-and-Guts" kutokana na ujasiri wake.
Chanzo BBC Swahili
0 on: " Trump amteua Jenarali James Mattis kuwa waziri wa ulinzi "