visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Friday, December 9, 2016

Bashar Assad asisitiza kushindwa njama za Magharibi huko Syria na katika eneo

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Al Watan, Rais wa Syria amesema kuwa Halab au kwa jina jingine Aleppo ndilo tumaini la mwisho la magaidi nchini humo baada ya kushindwa kwao huko Damascus na Homs na kwamba kukombolewa kikamilifu mji huo kutabadili mwenendo wa vita huko Syria.
Rais Bashar Assad amesisitiza namna serikali yake ilivyoamua kuyakomboa maeneo yote yanayoshikiliwa na magaidi nchini humo na kuongeza kuwa, Aleppo ni miongoni mwa maeneo hayo ambayo ni lazima yakombolewe yote.  Rais wa Syria amebainisha kuwa kuukomboa mji huo ni kwa maana ya kuvunja njama  na mipango ya Wamagharibi na waungaji mkono wao katika eneo hilo. Jeshi la Syria siku kadhaa zilizopita limepata mafanikio makubwa mashariki mwa mji wa Aleppo. Jeshi hilo lilianza oparesheni zake  za kuwafurusha  magaidi huko mashariki mwa Aleppo katikati ya mwezi Novemba uliopita. Syria ilikumbwa na mgogoro tangu mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi kuanzisha hujuma kubwa nchini humo kwa kuungwa mkono kwa hali na mali na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao lengo likiwa ni kuing'oa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al Assad.
Rais Bashar Assad wa Syria katika mahojiano na gazeti la al Watan 
Matukio ya kimaidani huko Syria yanaonyesha namna jeshi la nchi hiyo na makundi ya kujitolea ya wananchi yanavyotoa kipigo kikali kwa magaidi. Mafanikio makubwa waliyopata wananchi wa Syria  katika maeneo mbalimbali ya Syria khususan huko Aleppo katika mapambano dhidi ya magaidi ambao wanaungwa mkono pakubwa na nchi za Magharibi  na baadhi ya nchi za Kiarabu pamoja na Uturuki, yamevuruga mahesabu ya magaidi hao na waungaji mkono wao nchini humo. Matukio yanayojiri Syria  yanaonyesha kubadilika pakubwa mlingano wa nguvu katika oparesheni na kwenye medani kwa maslahi ya kujitawala wananchi wa nchi hiyo, na yanadhihirisha pia mafanikio makubwa ya jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Syria mbele ya magaidi. 
Kipigo kikali walichopata magaidi huko Aleppo kimesababisha kukaribia kukombolewa kikamilifu mji huo wa kistratijia na kihistoria, jambo ambalo limewatia wasiwasi mkubwa magaidi na waitifaki wao wasijue la kufanya. Kusonga mbele kwa haraka jeshi la Syria huko Aleppo, eneo ambalo linahesabiwa kuwa nukta nyingine muhimu katika muqawama unaoendeshwa na wananchi wa Syria dhidi ya magaidi, hakujasalia tu katika uwanja wa vita pekee, bali kusonga mbele huko kumekuwa na taathira katika uga wa kisiasa na kimataifa pia. Moja ya mafaniko hayo tunaweza kuashiria kuimarika nafasi ya serikali halali ya Syria ambayo ingali ina uungaji mkono mkubwa nchini humo. Hasa ikitiliwa maananani kuwa mustakbali wa siasa za Syria unapasa kuainishwa na raia wenyewe wa nchi hiyo. Kutekelezwa njama dhidi ya Syria kunapasa kutathminiwa katika fremu ya uingiliaji wa nchi ajinabi katika eneo la Mashariki ya Kati kunakofanywa na nchi za Magharibi kwa shabaha ya kuzigawa nchi za eneo hili. 
Jeshi la Syria likiwa katika mji wa Aleppo baada ya kuwafurusha magaidi
Katika fremu hiyo Aleppo ukiwa mojawapo ya miji muhimu ya Syria umekuwa na nafasi ya kipeee katika mahesabu ya wapangaji njama dhidi ya nchi hiyo; ambao wanafuatilia mpango wa kuigawa Syria kwa kukalia kwa mabavu kikamilifu Aleppo na kisha kuubadili mji huo kuwa mji mkuu wa eneo eti lililojitenga  na Syria litakalokuwa chini ya udhibiti wa magaidi. Kwa vyovyote vile, kusimama kidete jeshi na wananchi wa Syria ambao pia wanaungwa mkono na wanamuqawama katika eneo hili la Mashariki ya Kati, kwa mara nyingine tena kumepelekea kugonga mwamba madola yanayopenda kujitanua katika eneo hili. 


0 on: " Bashar Assad asisitiza kushindwa njama za Magharibi huko Syria na katika eneo "