![]() |
Faru John alitoweka katika mbuga ya taifa miezi mitatu iliyopita. |
Waziri mkuu nchini Tannzania amewapa maafisa wa hifadhi ya wanyagapori nchini humo hadi leo Alhamisi, kueleza aliko faru mweusi maarufu kwa jina John.
Kassim Majaliwa alisema kuwa maafisa hao aidha wotatoa pembe ya faru huyo ikiwa kama amekufa au waseme aliko.
Faru huyo alitoweka katika mbuga ya taifa miezi mitatu iliyopita. Kuna ripoti kuwa maafisa hao walihusika na kuuzwa kwa John kwa zaidi ya dola 90,000
Idadi ya faru imepungua zaidi nchini Tanzania huku wengi wakiuawa na wawindaji haramu ambao huuza pembe zao kwenda mataifa ya Asia
0 on: " Maafisa wapewa hadi leo kusema aliko faru John Tanzania "