Maafisa wa polisi nchini Korea Kusini wanasema kuwa wamemkamata mtu anayetuhumiwa kulichoma moto eneo alilozaliwa babake rais wa Taifa hilo Park Geun -hye.
Eneo hilo la kumbukumbu za Park Chung-hee ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi liliharibika vibaya kutokana na moto huo.
Polisi wamemnukuu mshukiwa akisema kuwa rais huyo angejiuzulu ama hata kuuawa kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Bi Park anakabiliwa na maandamano pamoja na kushtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufisadi.
Nyumba ambayo babake Park alizaliwa kusini mwa mji mwa Gumi, ni kivutio kikubwa cha uchumi hususan miongoni mwa wafuasi wa familia ya Park.
0 on: " Eneo alilozaliwa babake rais wa Korea Kusini lachomwa "