Nigeria ndio mabingwa wa kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya nane baada ya kuishinda Cameroon 1-0 mbele ya mashabiki 40,000 mjini Younde.
Bao la dakika za mwisho lililofungwa na Desire Oparanozie lilitosha kuisaidia Nigeria kuhifadhi kombe hilo ambalo walilinyakua nchini Namibia miaka miwli iliopita.
Timu hiyo inayojulikana kama Super Falcons ilitawala mashindano hayo ,kwa kushinda mechi zote walizocheza.
Katika marudio ya fainali za mwaka 2014, Cameroon ilimaliza wa pili kwa mara nyengine licha ya kupata ushabiki mkubwa kutoka nyumbani
Mbele ya rais wa Cameroon Paul Biya ,timu hiyo ya nyumbani ilitawala mechi hiyo kunako kipindi cha kwanza huku mshambuliaji Aboudi Obguene akipata nafasi za kutosha kuiweka mbele Cameroon lakini bila mafanikio yoyote.
Katika kipindi cha pili,Oparanozie, ambaye aliifungia Nigeria bao la ushindi dhidi ya Afrika Kusini katika mechi ya nusu fainali, alifunga bao hilo la pekee ikiwa imesalia dakika 7 mechi kukamilika.
0 on: " Nigeria yachukua ubingwa kombe la mataifa ya Afrika "