visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Thursday, December 8, 2016

Mazoezi kwa wanaume huongeza mbegu za uzazi

Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi kwa kiwango cha wastani.
Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi
Wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati , mbegu zao huwa na afya njema, kulingana na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi.
Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani , kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume.
Utafiti umebaini kwamba wale wanaoshiriki katika michezo kama vile ya uendeshaji baiskeli wanauwezo wa kupunguza kiwango cha mbegu zao za uzazi.
Mbinu za kuongeza mbegu za kiume:
  • Weka korodani katika madhari mazuri, kwa kuepuka kuvalia suari za ndani za kukaza.
  • Usioge na maji moto sana.
  • Epuka magonjwa ya zinaa.
  • Wacha uvutaji wa sigara.
  • Punguza kiwango cha pombe.
  • Usinone sana.
  • Fanya mazoezi, lakini kwa kiwango cha wastani.
Wanaume wote 261 waliosajiliwa katika majaribio hao hawakuwa na matatizo yoyote ya kiafya au shida ya uzazi. Walikuwa na kiwango sawa cha bengu za uzazi na zilizokuwa na afya, na walioishi maisha bila kufanya mazoezi.
Wanaume hao walishirikishwa kwenye mradi mmoja kati ya miradi minne ikiwemo:
  • Kutofanya mazoezi
  • Mazoezi makali mara tatu kwa wiki (dakika moja ya mbio ya kasi na mapumizo mafupi katika kila dakika kumi)
  • Mazoezi wa wastani mara tatu kwa wiki ( dakika 30 katika mashine ya kufanyia mazoezi)
  • Mazoezi makali , mara tatu kwa wiki( kwa karibu saa moja katika mashine ya kufanyia mazoezi)

    Chanzo BBC Swahili

0 on: " Mazoezi kwa wanaume huongeza mbegu za uzazi "