visitors

display number of visitors
Theme images by Storman. Powered by Blogger.
Showing posts with label Maajabu. Show all posts
Showing posts with label Maajabu. Show all posts

Saturday, February 11, 2017

Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii

- No comments
Mkalimani katika mbuga ya wanyama pori nchini Tanzania amekamatwa baada ya kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii mmoja kuhusu nchi na watu wake.
Kwenye video iliyosambazwa kwa wingi, mkalimani huyo anasema kuwa mtalii huyo anataka watu wa Tanzania waache kulalamika kwa sababu ya njaa
Ukweli ni kwamba mwananke huyo anasema kuwa wata wa Tanzania ni wazuri kupindukia.
Alikamatwa siku ya Alhamisi kwa agizo la waziri wa utalii.
Mkalimani huyo ambaye hakutajwa jina ni kutoka mbuga ya Serengeti iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.
Kamanda wa polisi eneo hilo Philipo Kalangi, aliiambai BBC kuwa anahojiwa lakini hakutoa habari za kina.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Video hiyo iliyochapishwa na gazeti la Kenya, mtalii anasema:
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
Chanzo BBC Swahili

Saturday, December 10, 2016

Sokwe mvuta sigara awasili Kenya

- No comments
Baada ya kutengenishwa na mamake muda mfupi baada ya kuzaliwa, sokwe Manno alisafirishwa hadi nchini Iraq ambapo aliishi akivuta sigara alizokuwa akipewa na wageni huku akipigwa picha na wageni waliokuwa wakimtembelea.
Sokwe huyo mwenye umri wa miak minne pia angevalishwa nguo kama mtoto na kupewa vinjwaji na peremende
Kisha ukakuja msaada kutoka kwa makundi kadha ya kutunza wanyama, na sasa siku za Manno kama mvutaji sigara zimwekwisha baada ya kuwasili katika kituo cha kuwatunza sokwe kilicho nchini Kenya wiki moja iliyopita.
Wakati wa safari kati ya Dohuk na Erbil nchini Iraq watu waliokuwa wakimsafirisha walikuwa umbalia wa kilomita 20 kutoka mji wa Mosul ambapo kuna mapigano makali kati ya jeshi la Iraq na kundi la Islamic State.
Baada ya siku kadha za safari akiwa amefungiwa kwenye kisanduku kidogo, Manno aliwasili katima kituo cha Ol Pejeta mnamo Novemba 30 ambacho kimekuwa kikiwatuza sokwe walio kwemye hatari wa kuangamia tangu mwaka 1993.


Thursday, December 8, 2016

Mwanamke mwenye kilo 500 kupelekwa India kufanyiwa upasuaji

- No comments
Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.
Mwanamke mmoja raia wa Misri anayeaminiwa kuwa mtu mzito zaidi duniani akiwa na kilo 500, hivi karibuni atasafirishwa kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wake.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36, atasafirishwa kwa ndege ya kukodishwa kwenda mjini Mumbai, ambapo daktari Muffazal Lakdawala, anapanga kumfanyia upasuaji.
Ubalozi wa India mjini Cairo ulikuwa umemnyima visa kwa kuwa hakuweza kufika kwenye ubalozi huo yeye binafsi.
Hata hivyo hali ilibadilika baada ya daktari kutoka mji wa Mumbia kuindikia kwa wizara ya mashauri ya kigeni ya India kupitia mtandao wa Twitter.
Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.
Ikiwa madai kuhusu uzito wake ni ya ukweli basi atakuwa mtu mzito zaidi duniani aliye hai kwa kuwa Pauline Potterraia raia ndiye anashikia rekosi ya Guinness
Alikuwa na kilo 292 mwaka 2010.


Monday, December 5, 2016

Wagonjwa wenye matatizo ya kiakili waikimbia hospitali Kenya

- No comments
Wagonjwa wenye matatizo ya kiakili waikimbia hospitali Kenya
Wagonjwa kadha wenye matatizo ya kiakili wameitoroka hospitali kuu ya wagonjwa wenye matatizo ya kiakili nchini Kenya, hospitali ya Mathari jijini Nairobi.
Taarifa za vyombo vya habari zinasema huenda wagonjwa hao wametumia fursa ya kutokuwepo kwa madaktari wanaogoma kutoroka.
Polisi wanawasaka wagonjwa hao.
Gazeti la Nation linasema wagonjwa waliotoroka ni karibu 50 ingawa Standard linaripoti kwamba huenda wakafikia 100.
Madaktari na wauguzi kote nchini Kenya wanagoma kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizi ya nyongeza ya mishahara na marupurupu mengine chini ya makubaliano yaliyotiwa saini Juni mwaka 2013.
Mgomo huo umeathiri hospitali zote zinazoendeshwa na serikali za majimbo pamoja na hospitali kuu za rufaa - Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Moi mjini Eldoret.
Maafisa wakuu wa afya serikali walifanya mkutano wa dharura Jumapili usiku kujaribu kuzuia mgomo huo lakini juhudi zao hazikufua dafu.


Wednesday, November 30, 2016

Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa Tanzania

- No comments
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kusini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani

Friday, November 25, 2016

Uhaba mkubwa wa wafungwa waikumba Uholanzi

- No comments
Huku maeneo mengi ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa kupita kiasi, Uholanzi ina tatizo tofauti. Uhaba wa wafungwa.
Katika kipindi cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake na mengine zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili liliwezekana - na kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya mahabusu na katika jengo zima. Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao cha jioni. Mwanamume mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliyofungwa juu.
"Hawawezi kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel, naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "
"Lakini wanaweza kuazima visu vidogo vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini."
Baadhi ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya kawaida mara baada ya kufunguliwa
Soma zaidi BBC Swahili