visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Thursday, December 8, 2016

Ndege yaanguka ikiwa na abiria 48 Pakistan

Mabaki ya ndege yakiteketea eneo la ajali
Ndege mmoja ya shirika la ndege Pakistan (PIA) iliyokuwa imewabeba abiria 48 imeanguka kaskazini mwa nchi hiyo.
Ndege hiyo aina ya PK-661, ilipoteza mawasiliano na mnara wa waelekezi wa ndege ilipokuwa ikitoka Chitral ikielekea Islamabad muda mfupi baada ya kupaa angani,'' shirika hilo limesema katika taarifa yake.
Ndege hiyo ya taifa imelaumiwa kwa kukosa kuimarisha usalama kwa siku za hivi karibuni.
Ajali kubwa ilitokea mwaka 2006 iliowaua watu 44.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Havelian, karibu kilomita 70 (maili 43) kaskazini mwa Islamabad kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Chanzo BBC Swahili


0 on: " Ndege yaanguka ikiwa na abiria 48 Pakistan "