Rais wa Tanzania John Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi rais wa Cuba Raul
Catsro kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Cuba Fidel
Castro. Katika salamu hizo magufuli
amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
kifo cha Fidel Castro. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Magufuli amesema
kuwa kwa niaba yake pamoja na wananchi wa taifa la
tanzania ametoa pole kwa wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu. Amemsifu
Fidel
kwa kuwa kiongozi sahupavu ambaye atakumbukwa kwa mchango
wake mkubwa katika ukombozi wa nchini za Kusini mwa Afrika pamoja na misaada
mikubwa aliyotoa kuboresha huduma zas kijamii kwa wananchi.
''Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima,historia ya
Tanzania haiwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro .Hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba
bali pia kwa Tanzania na Afrika'',alisema Magufuli.
0 on: " Raisi Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa raisi wa Cuba Raul Catsro kufuatia kifo cha Fidel Castro "