![]() |
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye |
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ameliomba bunge la nchi hiyo kutafuta njia ya kumuwezesha kuondoka madarakani, baada yake kukumbwa na kashfa ya ufisadi.
Amesema anataka bunge limsaidie kpata njia bora zaidi ya kuondoka madarakani bila kuacha pengo au kuzua mzozo wa kisiasa.
Bi Park amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ang'atuke huku uchunguzi wa iwapo alimruhusu rafiki yake ya muda mrefu kuwa na usemi kuhusu uamuzi wa kisiasa kwa manufaa yake binafsi ukiendelea.
Kiongozi huyo amesema ataachia "bunge kila kitu kuhusu mustakabali wangu, ikiwemo kufupisha muhula wangu", lakini hataki kuacha pengo uongozini.
Bunge lilikuwa limepangiwa kujadili iwapo anafaa kuondolewa madarakani Ijumaa.
Baadhi ya viongozi katika chama tawala walikuwa wamesema alifaa kung'atuka "kwa heshima" kabla ya mambo kufikia hatua ya sasa
0 on: " Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye tayari kujiuzulu "