![]() |
Philippe Coutinho |
Mchana wa November 28 2016 kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho alipelekwa hospitali na alifanyiwa vipimo vya afya vya mwisho, ili kujua jeraha lake la kifundo cha mguu litamuweka nje ya uwanja kwa muda gani.
Kiungo huyo wa kibrazil taarifa ya vipimo vyake imetoka na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6 kufuatia kuumia kifundo cha mguu, Coutinho aliumia katika mchezo wa Ligi KuuEngland dhidi ya Sunderland, uliyochezwa Jumamosi ya November 26 na kumalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Liverpool watamkosa staa huyo katika michezo 7 ya Ligi Kuu England, mechi ambazo Bournemouth (Dec 4), West Ham (Dec 11th), Middlesbrough (Dec 14th),Everton (Dec 19th), Stoke City (Dec 27), Man City (Dec 31) na Sunderland (Jan 2),Coutinho anatazamiwa kurudi uwanjani January 15 2017.
0 on: " Philippe Coutinho hatocheza michezo 7 ya Ligi Kuu England baada ya kupata jereha "