visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Sunday, November 27, 2016

Fidel Castro afariki dunia akiwa na umri wa miaka 90


Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake ametangaza.
"Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT Jumamosi)," Rais Raul Castro ametangaza.
Serikali imetangaza siku tisa za maombolezo ya kitaifa.
Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.
Wakati wa utawala wake, alisaidia sana mataifa ya Afrika, hawa makundi yaliyokuwa yakipigania uhuru Angola na Msumbiji.
Aidha, alikuwa akituma usaidizi wa matabibu na wataalamu, karibuni zaidi ikiwa nchini Sierra Leone wakati wa mlipuko wa Ebola.
Wafuasi wake walisema alikuwa ameirejesha Cuba kwa wananchi.
Lakini alituhumiwa pia kwa kuwakandamiza wapinzani.
Chini ya uongozi wa Fidel Castro, Cuba ilikuwa na uhusiano maalum na Afrika.
Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.
Fidel Castro aliongoza mapinduzi ya Kikomunisti Cuba mwaka 1959







Soma zaidi BBC Swahili




0 on: " Fidel Castro afariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 "