![]() |
Rais Lungu na Raisi Magufuli |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya mapokezi wawili hao waliketi kwa mazungumzo maalum yaliyokita katika kuendeleza miradi mbalimbali iliyoanzishwa na nchi hizo mbili ikiwemo reli (TAZARA) na bomba la mafuta (TAZAMA) ili iweze kuleta tija kwa wananchi
Lungu ataendelea na ziara yake hapa nchini ambapo pamoja na kutembelea miradi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ikiwemo TAZARA na TAZAMA, atashuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia
![]() |
Mhe. Edgar Chagwa Lungu akihutubia |
0 on: " Rais Magufuli akutana na Rais Lungu wa Zambia Ikulu "