Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua hatamu Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa $1 pekee kila mwaka.
Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.
Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.
Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."
0 on: " Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 "