visitors

display number of visitors
Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Tuesday, December 27, 2016

Watu 30 wafariki baada ya boti yao kuzama Uganda

- No comments
Ziwa Albert ambapo takriban watu 30 wanadaiwa kufa maji
Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo.
Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
Mafisa wa polisi wanasema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta.
Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia .
Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.


Watu 11 wauawa kwenye sikukuu ya Krismas, Marekani

- No comments
Watu 11 wameuawa katika mashambulio ya risasi kwenye mkesha na sikukuu ya Krismas mjini Chicago Marekani.
Polisi nchini humo wamesema pia kwamba watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyohusisha bunduki, na kuyahusisha na magenge ya uhalifu.
Idadi hiyo ya watu waliouawa imefanya jumla ya watu waliouawa kwa risasi katika kipindi cha mwaka 2016 kufikia mia saba na hamsini. Na kufanya mji huo kuongoza kwa mauaji katika kipindi cha miongo miwili.


Thursday, December 22, 2016

Petra Kvitova ashambuliwa kwa kisu

- No comments
Petra Kvitova
Bingwa wa zamani wa mchezo wa Tennis Wimbledon, Petra Kvitova, amefanyiwa upasuaji kwenye mkono wake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa kisu katika moja ya miji ya Jamhuri ya Chekslovakia.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa kijamii , ameeleza kuwa alishtushwa na shambulizi hilo na anajiona ana bahati kuwa hai baada ya kujitetea mwenyewe dhidi ya shambulizi hilo.
Msemaji wa bingwa huyo wa zamani ambaye anapewa nafasi ya kumi na moja kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi, amesema kwamba, afya ya bingwa huyo itatengamaa baada ya miezi mitatu.
Petra Kvitova aliwahi kuwa bingwa mchezo wa tenisi wa Wimbledon mwaka wa 2011 na 2014.


Leicester yashinda tuzo la klabu bora ya mwaka Uingereza

- No comments
Klabu ya soka ya Leicester imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa kuwashangaza wengi waliposhinda ligi ya Uingereza.
The Foxes kama inavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo.
Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa katika ligi ya Uingereza mwaka 2014-15.
Walipoteza mechi tatu pekee katika msimu wa 2015-16 na wamefuzu kucheza kombe la vilabu bingwa Ulaya na kuendelea hadi raundi za muondoano.
Mwanzoni mwa mwezi Aprili, Leicester ilikuwa pointi saba juu katika jedwali la ligi ya Uingereza .
Mwaka mmoja kabla ,walikuwa chini ya jedwali hilo pointi saba pekee juu ya timu ambazo zilishushwa daraja.