visitors

display number of visitors
Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Friday, September 8, 2017

MBOWE HALI YA TUNDU LISSU NI MBAYA SANA





Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na kupokea huduma ya kwanza na taarifa zinasema kuna mipango ya kumsafirisha hadi Nairobi kwa matibabu zaidi.
Rais wa Tanzania John Magufuli kupitia kwenye Twitter amesema amesikitishwa sana na kushambuliwa kwa mbunge huyo.
Ameandika: "Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria."
Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki akiwa nyumbani kwake.

0 on: " MBOWE HALI YA TUNDU LISSU NI MBAYA SANA "