visitors

display number of visitors
Theme images by Storman. Powered by Blogger.
Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Saturday, February 11, 2017

Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii

- No comments
Mkalimani katika mbuga ya wanyama pori nchini Tanzania amekamatwa baada ya kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii mmoja kuhusu nchi na watu wake.
Kwenye video iliyosambazwa kwa wingi, mkalimani huyo anasema kuwa mtalii huyo anataka watu wa Tanzania waache kulalamika kwa sababu ya njaa
Ukweli ni kwamba mwananke huyo anasema kuwa wata wa Tanzania ni wazuri kupindukia.
Alikamatwa siku ya Alhamisi kwa agizo la waziri wa utalii.
Mkalimani huyo ambaye hakutajwa jina ni kutoka mbuga ya Serengeti iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.
Kamanda wa polisi eneo hilo Philipo Kalangi, aliiambai BBC kuwa anahojiwa lakini hakutoa habari za kina.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Video hiyo iliyochapishwa na gazeti la Kenya, mtalii anasema:
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
Chanzo BBC Swahili

Tuesday, December 27, 2016

Watu 30 wafariki baada ya boti yao kuzama Uganda

- No comments
Ziwa Albert ambapo takriban watu 30 wanadaiwa kufa maji
Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo.
Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
Mafisa wa polisi wanasema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta.
Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia .
Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.


Watu 11 wauawa kwenye sikukuu ya Krismas, Marekani

- No comments
Watu 11 wameuawa katika mashambulio ya risasi kwenye mkesha na sikukuu ya Krismas mjini Chicago Marekani.
Polisi nchini humo wamesema pia kwamba watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyohusisha bunduki, na kuyahusisha na magenge ya uhalifu.
Idadi hiyo ya watu waliouawa imefanya jumla ya watu waliouawa kwa risasi katika kipindi cha mwaka 2016 kufikia mia saba na hamsini. Na kufanya mji huo kuongoza kwa mauaji katika kipindi cha miongo miwili.


Thursday, December 22, 2016

Maafisa wa Nigeria wamekamata mchele wa plastiki

- No comments
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.
Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".
Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.


Rais wa Gambia asema hang'atuki mamlakani ng'o

- No comments
Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Rais wa gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.
Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.
Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
Akiongezea: ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu.
Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia.
ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.
Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.
Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo manamo tarehe mosi mwezi Disemba ,lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha mungu.
Alisema kwamba matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.


Jamii ya kimataifa yamtaka Kabila kujiuzulu

- No comments
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anazidi kupokea shinikizo kimataifa kutokana na hatua ya kukataa kuachia maamlaka baada ya muhula wake wa kikatiba kukamilika jumatatu.
Ufaransa imesema itatuma ombi kwa umoja wa ulaya la kumwekea vikwazo iwapo ataendelea kushikilia maamlaka.
Ujerumani imehairisha majadiliano ya kuipa DR Congo msaada wa miradi ya maendeleo.