visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Tuesday, December 27, 2016

Watu 30 wafariki baada ya boti yao kuzama Uganda

- No comments
Ziwa Albert ambapo takriban watu 30 wanadaiwa kufa maji
Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo.
Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
Mafisa wa polisi wanasema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta.
Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia .
Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.


Watu 11 wauawa kwenye sikukuu ya Krismas, Marekani

- No comments
Watu 11 wameuawa katika mashambulio ya risasi kwenye mkesha na sikukuu ya Krismas mjini Chicago Marekani.
Polisi nchini humo wamesema pia kwamba watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyohusisha bunduki, na kuyahusisha na magenge ya uhalifu.
Idadi hiyo ya watu waliouawa imefanya jumla ya watu waliouawa kwa risasi katika kipindi cha mwaka 2016 kufikia mia saba na hamsini. Na kufanya mji huo kuongoza kwa mauaji katika kipindi cha miongo miwili.


Thursday, December 22, 2016

Petra Kvitova ashambuliwa kwa kisu

- No comments
Petra Kvitova
Bingwa wa zamani wa mchezo wa Tennis Wimbledon, Petra Kvitova, amefanyiwa upasuaji kwenye mkono wake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa kisu katika moja ya miji ya Jamhuri ya Chekslovakia.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa kijamii , ameeleza kuwa alishtushwa na shambulizi hilo na anajiona ana bahati kuwa hai baada ya kujitetea mwenyewe dhidi ya shambulizi hilo.
Msemaji wa bingwa huyo wa zamani ambaye anapewa nafasi ya kumi na moja kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi, amesema kwamba, afya ya bingwa huyo itatengamaa baada ya miezi mitatu.
Petra Kvitova aliwahi kuwa bingwa mchezo wa tenisi wa Wimbledon mwaka wa 2011 na 2014.


Leicester yashinda tuzo la klabu bora ya mwaka Uingereza

- No comments
Klabu ya soka ya Leicester imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa kuwashangaza wengi waliposhinda ligi ya Uingereza.
The Foxes kama inavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo.
Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa katika ligi ya Uingereza mwaka 2014-15.
Walipoteza mechi tatu pekee katika msimu wa 2015-16 na wamefuzu kucheza kombe la vilabu bingwa Ulaya na kuendelea hadi raundi za muondoano.
Mwanzoni mwa mwezi Aprili, Leicester ilikuwa pointi saba juu katika jedwali la ligi ya Uingereza .
Mwaka mmoja kabla ,walikuwa chini ya jedwali hilo pointi saba pekee juu ya timu ambazo zilishushwa daraja.

Maafisa wa Nigeria wamekamata mchele wa plastiki

- No comments
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.
Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".
Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.


Rais wa Gambia asema hang'atuki mamlakani ng'o

- No comments
Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Rais wa gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.
Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.
Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
Akiongezea: ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu.
Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia.
ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.
Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.
Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo manamo tarehe mosi mwezi Disemba ,lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha mungu.
Alisema kwamba matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.


Jamii ya kimataifa yamtaka Kabila kujiuzulu

- No comments
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anazidi kupokea shinikizo kimataifa kutokana na hatua ya kukataa kuachia maamlaka baada ya muhula wake wa kikatiba kukamilika jumatatu.
Ufaransa imesema itatuma ombi kwa umoja wa ulaya la kumwekea vikwazo iwapo ataendelea kushikilia maamlaka.
Ujerumani imehairisha majadiliano ya kuipa DR Congo msaada wa miradi ya maendeleo.


Monday, December 19, 2016

Darassa anusurika kifo kwenye ajali ya gari akiwa na meneja na director wake

- No comments


Video ikionesha mwanamuziki Darassa Baada ya kupata ajali
Mwanamuziki Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa Muziki amepata ajali akiwa na Mtayarishaji wa video Hanscana walipokuwa njiani wakirejea Dar es Salaam kutoka Kahama.
Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea eneo la Ntobo barabara ya kuelekea mgodi wa Bullyanhulu, Wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa wamenusurika kifo.

Sunday, December 18, 2016

Real Madrid yashinda kombe la klabu bingwa duniani

- No comments


Ronaldo na Benzema wakishereherekea ushindi wa klabu yao

Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick na kuinusuru Real Madrid kuishinda klabu ya Japan Kashima Antlers katika muda wa ziada ili kushinda taji la klabu bingwa duniani.
Real ilichukua uongoza kunako dakika ya tisa kupitia mshambuliaji Karim Benzema, lakini Gaku Shibasaki alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili ili kuiweka mbele Kashima.
Ronaldo hatahivyo alisawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya Lucas Vazquez kuchezewa visivyo na Shuto Yamamoto.

Wachezaji wa Kashima Antlers baada ya kupata bao dhidi ya Real Madrid
Mshindi huyo wa tuzo la Ballon d'Or baadaye aliiweka kifua mbele timu yake baada ya kupigiwa pasi nzuri na Benzema, kabla ya kukamilisha hat-trick yake dakika saba baadaye.
Ushindi huo unaipatia Real Madrid kombe la pili la klabu bingwa dunia na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika mechi zote hadi mechi 37.
Hatua hiyo ina maana kwamba washindi 10 wa taji hilo wanatoka bara Ulaya.


Mpiganaji wa IS awaua wanajeshi 48 Yemen

- No comments
Mpiganaji wa IS awaua wanajeshi 48 Yemen
Mshambuliaji wa kujitolea kufa katika mji wa bandarini Aden amewauwa wanajeshi 48 na kuwajeruhi wengine wengi.
Ripoti zinasema kwamba wanajeshi hao walikuwa wamepanga foleni kupokea mishahara yao karibu na kambi ya wanajeshi, wakati mshambuliaji huyo alipojilipua.
Wiki iliyopita, wapiganaji wa Islamic state waliwaua wanajeshi 50 mjini Aden, ambao wako chini ya udhibiti wa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Yemen.
Islamic State limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo linasema limewaua ''waasi'' 70.
Shambulio hilo linajiri wiki moja baada ya shambulio jingine kama hilo kuwaua wanajeshi 48 katika kambi hiyo


Waasi wachoma mabasi ya uokoaji watu Syria

- No comments
Mabasi ya kuwaokoa watu yamechomwa na waasi nchini Syria
Mabasi kadhaa yaliokuwa yakielekea kuwaokoa wagonjwa na watu waliojeruhiwa katika kijiji kinachomilikiwa na serikali katika mkoa wa Idlib nchini Syria yamechomwa na waasi.
Msafara huo ulikuwa ukielekea Foah na Kefraya maeneo yaliozungukwa na waasi.
Vikosi vinavyounga mkono serikali vinataka watu kuruhusiwa kuondoka katika kijiji cha Shia ili uokozi wa watu waliopo Allepo uanze.
Maelfu ya watu wanatarajia kuondoka .
Mpango wa awali wa kuwaondosha watu mashariki mwa Aleppo ulifeli siku ya Ijumaa, ukiwaacha raia wakiwa wamekwama katika vituo tofauti bila chakula na makao.

Saturday, December 17, 2016

Tanzania: Mwanzilishi wa Jamii Forums afikishwa kortini Dar es Salaam

- No comments

Mwanzilishi wa JamiiForums Maxence Melo, ambaye amekuwa akizuiliwa na maafisa wa polisi nchini Tanzania tangu Jumanne amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kushtakiwa kwa makosa matatu.
Makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini na kuzuia uchunguzi wa polisi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa Kimtandao.
Melo anadaiwa kusimamia anwani ya mtandao ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania kinyume na kifungu 79(c) cha Sheria za Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010, pamoja na kanuni za anwani za mtandaoni nambari 428 za mwaka 2011.
Nyaraka za mashtaka zinasema anwani ya mtandao ya jamiiforums.com ambayo haijasajiliwa chini ya kikoa cha anwani za Tanzania cha .tz.
Kwenye kosa jingine, ameshtakiwa kuzuia uchunguzi kinyume na kifungu 22(2) cha Sheria za Uhalifu wa Kimitandao ya mwaka 2015.
Nyaraka za mahakama zinasema "akiwa anafahamu kwamba jeshi la polisi lilikuwa linafanya uchunguzi wa jinai kuhusu mawasiliano ya kielektroniki kwenye mtandao wake, na akiwa na nia ya kuzuia uchunguzi, alikataa kutii agizo la kufichua maelezo aliyo nato."
Amepelekwa gereza la Keko mpaka Jumatatu.


Oscar kuzidi Messi na Ronaldo kwa kulipwa pesa nyingi

- No comments
Mchezaji wa Chelsea Oscar anatarajiwa kuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani atakapohamia Ligi Kuu ya Uchina mwezi Januari.
Shanghai SIPG wanatarajiwa kulipa £60m kumchukua kiungo huyo wa kati kutoka Brazil.
Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar, 25, ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai.
Taarifa zinasema atakuwa analipwa £400,000 kila wiki (£20.8m kila mwaka), ingawa huenda akapitwa haraka kwani kuna taarifa kwamba klabu za China zinajiandaa kulipa pesa nyingi kununua wachezaji wengine Januari. Mshahara wa Oscar ni sawa na £57,143 kila siku, au £2,381 kwa saa, au £39 kila dakika.
Kuna taarifa huenda Shanghai Shenhua ,ambao mkufunzi wao kwa sasa ni Gus Poyet aliyetoka Sunderland, wanapanga kumnunua nyota wa zamani wa Manchester United na Manchester City Carlos Tevez kutoka Boca Juniors. Tevez atakuwa analipwa £31.5m kila mwaka, sawa na £605,000 kila wiki.
France Football wanasema mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavaninaye huenda akahamia Tianjin Quanjian, walio chini ya beki wa zamani wa Italia Fabio Cannavaro, kwa euro 50m (£41.79m) fambapo atakuwa akilipwa £16.7m kila mwaka.
Mwenzake kwenye klabu Javier Pastore kutoka Argentina pia huenda akahamia China.
Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez pia amehushishwa na kuhamia Hebei China Fortune, ambayo mkufunzi wake kwa sasa ni aliyekuwa meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini. Sanchez, anatarajiwa kulipwa £500,000 kila wiki iwapo atakubali kuhama.






Klabu ambazo zimetumia pesa nyingi zaidi karibuni nchini China ni Shanghai SIPG, Jiangsu Suning, mabingwa wa ligi Guangzhou Evergrande Taobao na Shanghai Shenhua.
Chanzo BBC Swahili


Chelsea yaendeleza moto wake yaishinda Cyrstal Palace bao 1-0

- No comments
Diego Costa ndiye mfungaji bora wa ligi akiwa na mabao 13
Chelsea wamefungua mwaya wa pointi tisa baada ya kuwazima Crysral Palace na kusalia kileleni mwa jedwali la ligi.
Diego Costa aliwafungia Chelsea baada ya kuapata pasi safi kutoka kwa Cezar Azpilicueta.
Hata hivyo Palace noa walipoteza fursa nzuri baada ya Jason Pucheon kupoteza free Kick.
Chelsea wamemfuta Jose Mourinho kwa mara ya pili miezi saba baada ya kuwaongoza kushinda ligi.
Chelsea ambao walimalizi nafasi ya 10 mwaka 2015 wanaongaza kwa pointi 9 waking'ang'ania kushinda taji la tano.


Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Papua New Guinea

- No comments
Tetemeko kubwa la ardhi lenye uzito wa 7.9 katika vipimo vya richa ambalo lilikumba eneo la pwani ya Papua New Guinea linaonekana kusababisha uharibifu kidogo au kukosa kutosababisha uharibifu kabisa.
Wakaazi wengi wa pwani mwa nchi walianza kukimbia maeneo hayo.
Licha ya mawimbi kadha kuonekana sasa tangazo la tahadhari limetolewa.
Ni mitetemeko ya ardhi michache ya viwango kama hivyo hutokea duniani kila mwaka na nguvu za kuharibu za tetemeko hilo zinaonekana kupungua kutokana na umbali wake.

Malecela, Afisa mkuu wa NIMR aliyetangaza kuna Zika Tanzania afutwa kazi

- No comments
Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR), Dkt Mwele Malecela, ambaye alitangaza kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania, amefutwa kazi.
Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa inasema Rais wa John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo mkuu.
Taarifa hiyo hata hivyo haijaeleza sababu ya kufutwa kazi kwa Dkt Malecela, siku moja tu baada yake kutangaza kwamba kuna virusi hiyo.
Hata hivyo, kulikuwa kumetokea habari za kukinzana kutoka kwake na wizara ya afya kuhusu kuwepo kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Alitangaza kuwepo kwa virusi hivyo nchini Tanzania siku ya Alhamisi lakini Ijumaa, baada ya habari hizo kuenea kwenye vyombo vya habari, waziri wa afya Ummy Mwalimu akatoa taarifa kukanusha habari hizo.
"Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa na Dkt Mwele Malecela utatangazwa baadaye," taarifa hiyo inasema.
Dkt Mwele Malecela alikuwa ametangaza kwamba virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wake, virusi hivyo viligunduliwa wakati wa utafiti uliofanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Chanzo BBC Swahili


Zika Tanzania: Magufuli ateua mkuu mpya NIMR

- No comments
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Prof Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) saa chache baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa awali Dkt. Mwele Malecela.
Taarifa kutoka ikulu imesema uteuzi wa Prof Mgaya unaanza mara moja.
Dkt Mwele Malecela, alifutwa kazi siku moja tu baada yake kutangaza kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Taarifa ya kufutwa kwake, iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa, haikueleza sababu ya kufutwa kazi kwa Dkt Malecela,
Hata hivyo, kulikuwa kumetokea habari za kukinzana kutoka kwake na wizara ya afya kuhusu kuwepo kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Alitangaza kuwepo kwa virusi hivyo nchini Tanzania siku ya Alhamisi lakini Ijumaa, baada ya habari hizo kuenea kwenye vyombo vya habari, waziri wa afya Ummy Mwalimu akatoa taarifa kukanusha habari hizo.
Dkt Mwele Malecela alikuwa ametangaza kwamba virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Chanzo BBC Swahili


Thursday, December 15, 2016

Wakazi wa mji wa Aleppo wahamishwa

- No comments
Mabasi ishirini na magari ya wagonjwa kumi yanatumiwa katika zoezi la kuwahamisha wakazi wa mji wa Alepo nchini Syria kiwa ni pamoja na waasi pamoja familia zao, Waziri wa Ulinzi wa Urusi amebaini.
Kufuatia makubaliano kati ya serikali na waasi, watu waliojeruhiwa na familia zao ndio wameanza kuondoka na kisha waasi na familia zaopamoja na "wanamgambo 250" wasiokuwa na silaha wanapinga serikali, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Aidha, chanzo hicho kimesema, watu waliojeruhiwa na wagonjwa kutoka Foua na Kefraya, vijiji viwili vinavyokaliwa na Mashia wengi ambavyo vinadhibitiwa nawaasi katika mkoa jirani wa Idleb, pia watahamishwa katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali.
Wapiganaji 12000 na familia zao pia zoezi hilo linawahusu.
Kudhibitiwa kwa Aleppo na jeshi la serikali itakua pigo kubwa kwa waasi ambao walidhibiti sehemu ya mashariki ya mji wa pili wa Syria mwaka 2012, lakini leo wanajikuta wameangamizwa baada ya mashambulizi makali ya jeshi la serikali yaliyozinduliwa katikati mwa mwezi Novemba .
Rais wa Syria Bashar Al Assad anatazamiwa kuhutubia wananchi mjini Aleppo Alhamisi hii.

Mfalme wa Uganda kupata mpishi Jela

- No comments
Mfalme Charles Mumbere
Mfalme wa Uganda anayekabiliwa na mashtaka ya ugaidi amekubaliwa kuwa na mpishi binafsi na 'Fridge' ndogo kwenye chumba chake korokoroni. Amri hii imetolewa na mahakama. Charles Mumbere, Mfalme wa Rwenzururu amekubaliwa kupata huduma hii kwa sababu za kiafya; anaugua shinikizo la damu na kisukari.
Hata hivyo mamlaka za Uganda zimesema mfalme huyo hatakubaliwa kuwa na mpishi kutoka nje. Mfalme Mumbere alikamatwa mwezi uliopita baada ya maafisa wa usalama kuvamia Kasri lake Magharibi mwa Uganda wilaya ya Kasese. Zaidi ya watu 80 waliuawa kwenye makabiliano hayo.
Kiongozi huyo wa kijamii amekanusha kuhusika na ghasia hizo. Alikamatwa pamoja na wafuasi wake 150 waliojumuisha walinzi wake. Wakili wake, Caleb Alaka ameambia BBC kwamba lazima maafisa wa jela waheshimu uwamuzi wa mahakama. Alaka amesema wapishi wengi wa mfalme waliangamia wakati wa uvamizi huo. Mfalme huyo atakubali mpishi atakayesajiliwa na maafisa wa jela.
Hata hivyo kumetokea na taarifa kwamba vyumba vya gereza havina umeme wala eneo la kuweka 'Fridge'. Mfalme huyo anazuiliwa katika jela kuu la Luzira mjini Kampala. Haijabainika ikiwa mashtaka ya ugaidi yanahusisha operesheni ya kijeshi iliyofanyika Kasri lake au mauaji ya afisa wa polisi hapo mwezi Machi.Mfalme huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena tarehe 28 mwezi Machi mwakani.
Serikali ya Uganda imelaumu Ufalme wa Rwenzururu ulioko wilaya ya Kasese kwa kuwasajili na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wakiwa na nia ya kujiondoa kutoka kwa Uganda na kuunda taifa lao huru kwa jina Yira.
Eneo hilo lililoko katika mpaka wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekumbwa na ghasia kati ya jeshi na makundi yenye silaha. Makabiliano hayo yamesababisha mauaji ya wanajeshi na hata raia. Kabla ya kutawazwa Mfalme, Charles Mumbere aliishi kwa miaka mingi nchini Marekani, ambapo alihudumu katika nyumba ya wazee jimbo la Pennsylvania

Binti wa rais wa zamani wa Msumbiji auawa

- No comments
Valentina Guebuza

Binti wa Rais wa zamani nchini Msumbiji, Armando Guebuza, Valentina Guebuza ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Maputo. Mumewe, Zofino Muiuane amekamatwa na polisi kufuatia tukio hilo lililofanyika Jumatano.
Bi Guebuza alikua na umri wa miaka 36 na imeripotiwa alipigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na majeraha wakati akipelekwa hospitalini.Mumewe alikamatwa katika moja wapo ya maeneo ya burudani mjini Maputo, kwa mujibu wa gazeti moja.
Valentina Guebuza aliorodheshwa nafasi ya saba miongoni mwa wanawake chipukizi wenye ushawishi Barani Afrika na jarida la Forbes mwaka wa 2013. Alishikilia nafasi ya juu katika kampuni kadhaa za mawasiliano pamoja na biashara zinazomilikiwa na familia.
Mumewe bwana Muiuane ni mfanyibiashara na aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya sigara ya 'British American Tobacco'. Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2014 kwenye sherehe iliyohuhduriwa na wageni 1,700 akiwemo Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Mfalme wa Zwaziland Mswati wa Tatu na binti wa Rais wa Angola Isabel dos Santos. Walijaaliwa na mtoto wa kike mwaka uliopita. Armando Guebuza alistaafu kama Rais mwaka wa 2014 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.


Oscar: Kiungo wa Chelsea kuhamia China

- No comments
Oscar amechezea Chelsea mechi 202 tangu ajiunge nao 2012
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amesema ana "uhakika 90% certain" kwamba atahamia klabu ya Shanghai SIPG inayocheza Ligi Kuu ya China kipindi cha kuhama wachezaji Januari.
Inakadiriwa kwamba mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 atanunuliwa takriban £60m.
Alijiunga na Chelsea kutoka Internacional kwa £25m mwaka 2012.
Oscar alianza kwenye mechi tano za kwanza chini ya Antonio Conte lakini amechezeshwa mara nne pekee tangu Septemba.
"Inategemea mambo kadha tu ya urasmi," Oscar aliambia Sportv ya Brazil.
Conte hakukanusha madai ya Oscar alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake baada ya ushindi wa Chelsea wa 1-0 dhidi ya Sunderland Jumatano.
Amesema hali ya Oscar itakuwa wazi zaidi siku chache zijazo.
Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai.
Oscar amechezea Chelsea mechi 202 na kufunga mabao 38.
Ameshinda Ligi ya Premia, Europa League na Kombe la Ligi.


Ligi ya soka DR Congo yasitishwa

- No comments
TP Mazembe ndio mabingwa watetezi wa ligi DR Congo
TP Mazembe ndio mabingwa watetezi wa ligi DR Congo
Ligi ya kandanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imesitishwa kwa muda usiojulikana kutokana na sababu za kiusalama.
Serikali ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia Alhamisi.
Hatua hiyo imetokea huku wasiwasi ukiendelea kwamba huenda kukatokea vurugu muhula wa Rais Joseph Kabila utakapofikia kikomo wiki ijayo.
"Hali iliyopo nchini huenda ikafika viwanjani," Barthelemy Okito, katibu mkuu wa wizara ya michezo alisema.
Majuzi wakati wa mechi, mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika.
Kabila alitakiwa kung'atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi jana.