visitors

display number of visitors

Blog Archive

Theme images by Storman. Powered by Blogger.

Wednesday, November 30, 2016

Majivu ya Fidel Castro kusafirishwa Santiago

- No comments
Mji wa Santiago unaojulikana kama chimbuko la ukomunisti wa Cuba, ndiko mapinduzi yaliyoongozwa na marehemu Castro yalianzia mnamo mwaka 1953 na akachukua urais mwaka 1959.
Baada ya mamia ya maelfu ya watu kuhudhuria misa ya wafu kwa mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro, majivu ya marehemu huyo yanaanza kusafirishwa leo kutoka jiji kuu Havana hadi Santiago kufanyiwa mazishi hapo siku ya Jumapili. Huo ukiwa umbali wa kilomita 900. Maelfu kwa maelfu ya wacuba wanatarajiwa kuwa barabarani kushuhudia majivu hayo yatakapokuwa yakisafirishwa. 
Mwili wa Fidel Castro aliyefariki akiwa na umri wa miaka 90, Ijumaa wiki jana, ulichomwa moto kulingana na matakwa yake. Majivu yake yatapitishwa katika miji kadhaa nchini humo kwa siku tatu kwanzia leo, kabla ya kufikishwa mji wa Santiago ambako ndiko atazikwa siku ya Jumapili.
Mji wa Santiago unaojulikana kama chimbuko la ukomunisti wa Cuba, ndiko mapinduzi yaliyoongozwa na marehemu Castro yalianzia mnamo mwaka 1953 na akachukua urais mwaka 1959.  Hapo jana mamia ya maelfu ya waombolezaji walifika kumpa heshima za mwisho jijini Havana.
Rais wa Bolivia ni miongoni mwa waliohudhuria misa hiyo na alisema: "Fidel hajafa kwa sababu wanaopigania uhuru hawafariki. Huyo ni Fidel. Hajafa kwa kuwa mawazo hayafi hasa mawazo yanayoleta ukombozi. Fidel hajafa kwa kuwa mapigano hayajaisha hasa mapigano dhidi ya utengano. Fidel ni kama yuko hai kuliko zamani akiendeleza vita kuokoa makazi yetu ya pamoja".
Mazishi yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa wakiwemo marais Nicolas Maduro wa Venezuela, Daniel Ortega wa Nicaragua, Evo Morales wa Bolivia na Rafael Correa wa Equador, kando na wakuu wa nchi za Amerika ya kusini na mfalme wa zamani wa Uhispania Juan Carlos.
Uhusiano wa Cuba na Marekani
Fidel Castro alitawala Cuba kwa miaka 47, hadi alipojiuzulu mwaka 2006 kufuatia hali yake ya kiafya, na kumkabidhi nduguye Raul Castro. Tangu wakati huo hajajitokeza hadharani japo inaaminika alikuwa na wasiwasi na uhusiano ulioimarishwa mwaka 2014 kati ya nchi yake na hasimu wao wa jadi Marekani. Haijabainika ikiwa uhusiano huo utaendelea kuimarika baada ya Januari rais mteule wa Marekani Donald Trump atakapochukua rasmi urais
Akitoa hotuba ya rambirambi jijini Havana, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema "Cuba haikutafuta madini ya dhahabu, almasi au mafuta barani Afrika. Wacuba walitaka uhuru na mwisho wa unyanyasaji wa bara la Afrika kutumiwa kama kiwanja cha kuchezewa na nchi kubwakubwa huku watu wakiteseka".
Fidel Castro alipendwa na wengi duniani hasa Amerika ya kusini na Afrika, kwa kusimama dhidi ya Marekani, huku akizindua mipango ya elimu bure na huduma za afya bila malipo kando na kuwatuma madakitari wao katika mataifa mengine duniani kutoa misaada ya kiafya.
Lakini wengine walimshutumu kuwa kiongozi wa kiimla aliyevuruga uchumi kutokana na sera zake za usosholisti na kuwanyima wacuba haki za kibinadamu mfano uhuru wa kujieleza.

Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa Tanzania

- No comments
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kusini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani

Rwanda kuwapeleleza askari 20 wa Ufaransa

- No comments
Ofisi ya mashitaka ya Rwanda imetangaza kuanza upelelezi kuhusu askari 20 wa nchi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Tangazo lililotolewa na ofisi ya mashitaka ya Rwanda linasema kwamba Rwanda imewasilisha maombi ya ushirikiano wa kisheria ili askari watuhumiwa waweze kuhojiwa na wapelelezi wa Rwanda.
Katika tangazo hilo Rwanda inasema kuwa imeanza rasmi mchakato wa kisheria kuhusu maafisa hao wanaotuhumiwa hukusika moja kwa moja katika mauaji ya kimbari.
Mwendesha mashitaka mkuu wa Rwanda Richard Muhumuza alimwandikia mwezake wa Ufaransa Jean Claude Marin kutaka ushirikiano wa kisheria kuwasaidia wapelelezi wa Rwanda kuwahoji maafisa hao wa Ufaransa kupitia ubalozi wa Rwanda mjini Paris.
Maafisa hao 20 ni miongoni mwa askari wa Ufaransa waliokuwa katika kazi mbali mbali nchini Rwanda kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 1994.
Rwanda inawatuhumu kulisaidia jeshi la rais wa zamani Juvenal Habyarimana kwa silaha na kutoa mafunzo kwa wanamgambo wa Interahamwe waliotekeleza mauaji ya kimbari.
Tangazo hilo linasema kwamba wakati wa upelelezi huo pia baadhi ya viongozi wengine au wajumbe wa serikali ya Ufaransa wanaweza kuombwa kutoa taarifa zinazoweza kusaidia mwendesha mashitaka.
Orodha ya maafisa hao 20 ilifanywa kwa kuzingatia ripoti mbali mbali zilizofanywa kuhusu nafasi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari.
Rwanda ilivunja uhusiano wake na Ufaransa mwaka 2006 baada ya jaji wa Ufaransa kutoa waranti za kuwakamata maafisa 10 wa jeshi la Rwanda kwa tuhuma za kudungua ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana,tukio ambalo linadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya kimbari.
Hata hivyo ziara ya aliyekuwa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy nchini Rwanda mwaka 2010 ilirejesha matumaini ya uhusiano mpya.
Hakuomba msamaha kwa niaba ya taifa lake lakini alikiri kuwepo makosa ya kisiasa yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa nchi yake ambayo hata hivyo hakufafanua.
Hivi karibuni Ufaransa ilitangaza hatua ya kurejelea upya upelelezi kuhusu aliyedungua ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana kwa kumhusisha mkuu wa zamani wa jeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa ambaye sasa ni mpinzani mkuu wa rais Kagame.
Hatua hii imekasirisha sana Serikali ya Rwanda ambapo Rais Paul Kagame alisema kuanza upya upelelezi huo ni kitendo cha uchokozi dhidi ya nchi yake baada ya upelelezi wa awali uliofanywa na Ufaransa yenyewe kubainisha kuwa ndege hiyo ilidunguliwa na wafwasi wakereketwa wa hayati Habyarimana;na kwamba nchi yake iko tayari kupigania hadhi yake

Marekani yakiri kuongoza mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Syria

- No comments

Marekani imekiri kufanya mashambulio mashariki mwa Syria yaliyowauwa makumi kadhaa ya vikosi vya serikali ya Syria vinvyopigana dhidi ya Islamic State (IS).

Muungano unaoongozwa na Marekani unasema kuwa lengo kuu la shambulio hilo ambalo limetajwa kama "kosa " la tarehe 17 Septemba lilikuwa ni kulenga mashambulio hayo katika ngome za Islamic State
Ndege za muungano huo kutoka mataifa ya Uingereza, Marekani, Denmark na Australia zilihusika katika shambulio hilo karibu na Deir al-Zour.
Rais wa Syria Bashar al-Assad alisisitiza kuwa shambulio hilo lililosababisha vifo vingi lilikuwa la makusudi.
Shambulio hilo ambalo jeshi la Urusi linasema kuwa liliwauwa watu wapatao 62, lilisitishwa baada ya Urusi kuifahamisha Marekani kwamba inawalenga wanajeshi wa Syria .
"Katika kisa kama hiki, hatukuweza kufikia kiwango chetu cha haiba tuliyonayo ,na tunaweza kufanya vyema kuliko hili," alisema Luteni Generali katika jeshi la Marekani Jeff Harrigian.
Msemaji wa kituo kikuu Marekani kinachotoa maagizo ya harakati za kijeshi za Marekani katika eneo la mashariki ya kati, amesema kosa la mashambulio hayo ni la "kujutia", na kuongeza kuwa haikuwa makusudi kulenga vikosi vya Syria
"Zilikuwa ni ndege nne zilizoendelea kushambulia ngome za majeshi ya Syria kwa karibu saa nzima, ama kwa muda wa zaidi kidogo ya saa moja ," Rais Assad aliliambia shirika la habari la AP mwezi Septemba.
Msemaji wa wizara ya usalama ya Uingereza alisema katika repoti iliyotolewa Jumanne kwamba uamuzi wa mashambulio hayo karibu na Deir al-Zour ulikuwa "wa nia njema ".
"Tunaafiki ripoti ya muungano na maazimio yake kwamba uamuzi wa kutambua maeneo ya kulenga mashambulio ya Daesh ya wapiganaji wa I-S ulikuwa na sababu ," alisema
" Tusingeweza na hatuwezi kufanya mashambulio ambayo yanafahamika kuwa ya ''vikosi vya utawala wa Syria'' kwa makusudi aliongeza .

Golikipa wa timu ya taifa ya Ghana awasili Tanzania kujiunga na Simba

- No comments
Daniel Nana Agyei
Golikipa wa timu ya taifa ya Ghana anayeichezea klabu ya Medeama ya kwao GhanaDaniel Nana Agyei amewasili Dar es Salaam Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mpango wake wa kujiunga na klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba.

Daniel anajiunga na Simba akiwa amewahi kuvitumikia vilabu vya Free State Stars ya Afrika Kusini, Liberty Professionals na Medeama SC zote za GhanaAgyei mwenye umri wa miaka 27 amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ghana mechi 5

Rais Magufuli azuru gereza la Ukonga ghafla

- No comments
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar -Es - Salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini humo na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi.
Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini mwake kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli''
Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini DSM.
Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.
Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini Tanzania.

Tuesday, November 29, 2016

DO NOT BITE MORE THAN YOU CAN CHEW

- No comments
Ebenezer Mollel

For quite some time, we have been witnessing an increasing tide of adopting local content as a critical tool in addressing the capacity gap in resource rich countries. A few countries have gone a step further to believe that local content could be a panacea for their poorly performing economies. As a result, some of these countries, without even identifying their current capacity and defining their position, would lay down unusually high local content requirements for the International Oil Companies to abide by. The existing cloud of mistrust between governments and foreign investors stands as a major reason as to why these two parties find themselves in a tug of war. Some host Governments have had the tendency of seeing the IOCs as looting vehicles that always look after a windfall profit. On the other hand, the IOCs, at some point, may see the Government as a potential threat that could drive them up the wall.
Read More. . .

Other Related articles published by Ebenezer Mollel

Philippe Coutinho hatocheza michezo 7 ya Ligi Kuu England baada ya kupata jereha

- No comments
Philippe Coutinho

Mchana wa November 28 2016 kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho alipelekwa hospitali na alifanyiwa vipimo vya afya vya mwisho, ili kujua jeraha lake la kifundo cha mguu litamuweka nje ya uwanja kwa muda gani.

Kiungo huyo wa kibrazil taarifa ya vipimo vyake imetoka na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6 kufuatia kuumia kifundo cha mguu, Coutinho aliumia katika mchezo wa Ligi KuuEngland dhidi ya Sunderland, uliyochezwa Jumamosi ya November 26 na kumalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Liverpool watamkosa staa huyo katika michezo 7 ya Ligi Kuu England, mechi ambazo Bournemouth (Dec 4), West Ham (Dec 11th), Middlesbrough (Dec 14th),Everton (Dec 19th), Stoke City (Dec 27), Man City (Dec 31) na Sunderland (Jan 2),Coutinho anatazamiwa kurudi uwanjani January 15 2017.

Jose Mourinho kuadhibiwa

- No comments
Jose Mourinho akipiga teke chupa ya maji
Chama cha soka cha nchini England FA, kimemfungulia mashitaka Meneja wa Manchester United Jose Mourinho kufuatia tukio la kupiga teke chupa za maji katika mchezo wa jumapili dhidi ya West Ham .
Taarifa ya FA imesema Mourinho alitenda kosa katika Dakika ya 27 ya mchezo uliomalizika kwa Sare ya 1-1.
Kocha huyu alionyesha kuchukizwa na kitendo cha mwamuzi Jonathan Moss,kutoipa timu yake mpira wa adhabu na badala yake kumpa ya njano Kadi Paul Pogba.
Mourinho amepewa muda wa mpaka Desemba Mosi kujibu mashitaka yanayomkabili, hii ni mara ya pili kwa kocha huyu msimu huu kuingia matatani na chama cha soka cha England.
Mara ya kwanza alikwaruzana na Mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo dhidi ya Burnley, ambapo alifungiwa mchezo na kutozwa faini

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye tayari kujiuzulu

- No comments

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye


















Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ameliomba bunge la nchi hiyo kutafuta njia ya kumuwezesha kuondoka madarakani, baada yake kukumbwa na kashfa ya ufisadi.
Amesema anataka bunge limsaidie kpata njia bora zaidi ya kuondoka madarakani bila kuacha pengo au kuzua mzozo wa kisiasa.
Bi Park amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ang'atuke huku uchunguzi wa iwapo alimruhusu rafiki yake ya muda mrefu kuwa na usemi kuhusu uamuzi wa kisiasa kwa manufaa yake binafsi ukiendelea.
Kiongozi huyo amesema ataachia "bunge kila kitu kuhusu mustakabali wangu, ikiwemo kufupisha muhula wangu", lakini hataki kuacha pengo uongozini.
Bunge lilikuwa limepangiwa kujadili iwapo anafaa kuondolewa madarakani Ijumaa.
Baadhi ya viongozi katika chama tawala walikuwa wamesema alifaa kung'atuka "kwa heshima" kabla ya mambo kufikia hatua ya sasa
Soma Zaidi BBC Swahili




Ndege iliyobeba wachezaji wa timu ya soka ya Brazil yaanguka Colombia

- No comments
Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.
Taarifa zinasema watu 25 wamethibitishwa kufariki na sita wamenusurika..Ndege hiyo inadaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.
Ndege hiyo ilikuwa safariki kutoka Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional.
Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo, la pili kwa umuhimu Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano lakini sasa imesitishwa.
Timu hito inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kulaza San Lorenzo ya Argentina.
Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.
Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema: "Tunamuomba Mungu awe na wachezaji, maafisa, wanahabari na wageni wengine watu ambao walikuwa wameandamana na ujumbe wetu."
Wamesema hawatatoa taarifa nyingine hadi ibainike kiwango kamili cha mkasa huo.
Taarifa zinasema watu wawili kutoka kwa timu hiyo - Alan Ruschel na Danilo - huenda wamenusurika.
Telemundo Deportes wameandika kwenye Twitter kwamba Ruschel ameathiriwa na mshtuko lakini ana fahamu na anazungumza. Aidha, ameomba aruhusiwe kukaa na pete yake ya harusi na awaombe jamaa zake.

Timu hiyo ilipangiwa kucheza mechi ya awamu ya kwanza ya fainali za Copa Sudamericana




















Ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya saa sita usiku saa za huko (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege, marubani walisema ndege hiyo ilikuwa imepata matatizo katika mfumo wake wa umeme.
Meya wa mji ulio karibu wa La Ceja amethibitisha kwamba mchezaji mmoja wa miaka 25 ni miongoni mwa manusura.



Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura.
Hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.
Hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura.









Mshambuliaji ajeruhi 11 katika shambulizi kwenye Chuo Kikuu cha Ohio

- No comments















Mwanafunzi wa kisomali kwenye chuo kikuu cha Ohio ameendesha gari yake kwenye mkusanyiko wa watembea kwa miguu Jumatatu na halafu kutoka nje ya gari na kuanza kuwachoma visu, akijeruhi watu 11.
Alipigwa risasi na kuuawa na polisi. Mkuu wa polisi wa Columbus, Kim Jacobs amesema wanaliona shambulizi hilo kuwa ni kitendo cha kigaidi.

Chuo kikuu cha Ohio kimemtaja mshambuliaji kuwa ni Abdul Razak Ali Artan, mwanafunzi katika chuo hicho. Wana jumuiya katika mji wa Columbus wameiambia VOA kuwa mwanamme huyo mwenye asili ya kisomali alikuwa na umri wa miaka 20.

Mwanafunzi mwenye jina kama hilo katika chuo hicho aliwahi kutajwa katika toleo la mwezi Agosti la gazeti la chuoni hapo akielezea wasi wasi wa kutokuwepo kwa vyumba vya kufanya ibada kwenye chuo kikuu hicho.

Maafisa hospitali wamesema hakuna muathirika aliyepata majeraha ya kutishia maisha yake. Rais wa chuo kikuu Michael Drake amesema kulikuwa na uvumi wa mshukiwa wa pili. Hata hivyo, Drake amesema polisi walifanya msako na wanaamini kulikuwa na mshambuliaji mmoja tu. Shirika la Upelelezi la FBI limejiunga katika uchunguzi.

Mshauri mkuu wa rais wa Burundi anusurika kuuawa mjini Bujumbura

- No comments

Willy Nyamitwe

Mshauri mkuu wa rais wa Burundi anayehusika na maswala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe ameponea kuuawa baada ya kundi la watu kushambulia gari lake alipokua akikaribia nyumbani kwake eneo la Kajaga Kilomita 7 kutoka mjini Bujumbura.

Willy Nyamitwe, Mshauri wa Rais Pierre Nkurunziza anayehusika na mawasiliano, ameponea kuuawa alipokua akikaribia kuwasili nyumbani kwake usiku wa Jumatatu Novemba 28, eneo la Kajag, mtaani Rukaramu mkoani Bujumbura vijijini, kilomita 7 na mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Askari mmoja mongoni mwa walinzi wake aliuawa na mwengine kujeruhiwa. Watu hao walioendesha shambulio hilo hawajajulikana.
Habari ambayo haijathibitishwa na serikali na imeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Burundi. Lakini inaarifiwa kuwa Willy Nyamitwe anapewa matibabi katika hospitali ya Kira Hospital mjini Bujumbura, baada ya kujeruhiwa kwa risasi mkononi.
Willy Nyamitwe ambaye ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala cha CNDD-FDD na utawala wa Pierre Nkurunziza amekua akilaumiwa na upinzani na mashirika ya kiraia yaliyo uhamishoni nje ya kuwa amekua akitoa maneno mabaya dhidi yao.
Hata hivyo Afisa huyo amekua akilaumi na baadhi ya wa fuasi wa chama tawala kwa kuendelea kuchochoea chuki inayolenga kukigawa chama hiki.
Chama cha CNDD-FDD kinaendelea kukabiliwa na malumbano ya ndani, ambapo baadhi ya wafuasi wanabaini kwamba chama hiki kinaongozwa na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi na polisi waliotoka katika chama hicho wakati kilipokua kikiendesha viuta vya maguguni wamesem akuwa wafuasi hawana kauli katika chama hicho.

Hali ya usalama imeendelea kudorora nchini Burundi, na machafuko yaliyoikumba nchi hiyo tangu rais Pierre Nkurunziza kuchuku uamuzi wa kuwania muhula mwengine, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 kwa mujibu wa mashirika ya kiraia, na watu zaidi ya 250,000 kuyakimbia makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.

Zimbabwe yazindua noti mpya

- No comments
Waandamanaji wakipinga utambulisho wa noti mpya nchini Zimbabwe
Zimbabwe imetangaza kuanza kutumia noti mpya, ikitoa noti ya dhamana za serikali ya dola milioni 10, ambazo zinatazamiwa kusaidia kupunguza matatizo makubwa ya upatikanaji wa fedha.
Matatizo ya kifedha yaliikumba nchi hiyo iliyo Kusini mwa Afrika na kupelekea kutumia fedha mbalimbali za nje ikiwemo dola ya Marekani tangu mwaka 2009; baada ya kiwango cha mfumko kufikia kilele chake kwa asilimia bilioni 500 na kusasabisha dola ya Zimbambwe kutokutumika.
Kutambulishwa kwa noti za dhamana za dola 2 na 5 katika mzunguko wa fedha kunafuatia pia kutambulishwa kwa sarafu ambazo zilianza kutumika mwaka mmoja uliopita ili kupunguza upungufu wa ubadilishaji fedha.
Zimbabwe imekumbwa na uhaba mkubwa wa dola ya Marekani katika miezi ya hivi karibuni, hali ambayo ilipelekea serikali ya raisi Robert Mugabe kuchapisha fedha ambayo imepewa jina la utani la fedha mbadala.
Wananchi wanapinga kutambulishwa kwa noti hizo mpya kwa sababu bado wanahasira na kuanguka kwa dola ya Zimbabwe, ambayo ilitelekezwa mwaka 2009, kutokana na mfumuko mkubwa wa bei anasema mhariri wa gazeti huru la wiki, the standard, na kuongeza kuwa serikali imekuwa na kiburi,na kuwatawanya wale ambao wamekuwa wakipinga fedha mbadala na kuonekana kuwa si wazalendo.
Utoaji fedha katika banki wadhibitiwa
Benki kuu nchini humo imefanya uzinduzi wa matangazo katika vyombo vya habari kujaribu kuwatisha watu na kusema kuwa wafanya biashara wadogo na wakubwa wamekubali utambulisho wa noti hizo, japo utambulisho wa noti hizo umezusha hofu ya upungufu wa mafuta katika vituo kwa wiki iliyopita na kusababisha msongamano mkubwa katika vituo vya kuuza mafuta.
Serikali kwa upande wake, imewataka madereva kutokuwa na wasiwasi na kusema kuwa kuna mafuta ya kutosha yamehifadhiwa, katika taarifa iliyotolewa wiki iliyopita serikali imesema "tunapenda kuwahakikishia kuwa nchi hakuna ukweli wowote wa madai kuwa nchi itakumbwa na uhaba wa mafuta"
Utoaji wa fedha banki unadhibitiwa ambapo sasa watumiaji wanaweza kutoa pesa kiwango cha juu cha dola 150 tu kwa wiki.
Uchumi wa nchi hiyo umeaanguka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni huku banki zikikumbwa na uhaba wa fedha hali ambayo iliwachanganya watumiaji wa huduma hizo na kuwalazimisha wengine kulala nje ya banki wakitaka kutoa pesa zao.
Utambulisho wa noti hizo umeamsha hasira ambazo zimesababisha kuibuka kwa waandamanaji mitaani, katika kipindi cha wiki mbili wanaharakati kadhaa walikamatwa na kupigwa kabla ya kufanyika kwa maandamano yaliyopangwa ili kupinga utambulisho wa noti hizo


Rais Magufuli akutana na Rais Lungu wa Zambia Ikulu

- No comments
Rais Lungu na Raisi  Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mara baada ya mapokezi wawili hao waliketi kwa mazungumzo maalum yaliyokita katika kuendeleza miradi mbalimbali iliyoanzishwa na nchi hizo mbili ikiwemo reli (TAZARA) na bomba la mafuta (TAZAMA) ili iweze kuleta tija kwa wananchi

Lungu ataendelea na ziara yake hapa nchini ambapo pamoja na kutembelea miradi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ikiwemo TAZARA na TAZAMA, atashuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia 

Mhe. Edgar Chagwa Lungu akihutubia

Ufafanuzi mzuri Kuhusu kauli ya Waziri Ndalichako kwa wanaojiunga Vyuo Vikuu

- No comments

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia wanafunzi wenye Stashahada (Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa, katazo lililotolewa na Waziri Prof. Ndalichako siku ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania linawahusi wale tu wanaosoma Foundation Courses ili kuweza kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu.
Taarifa imeeleza kuwa awali wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne walikuwa wakisoma Foundation Courses katika vyuo mbalimbali na kisha kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu kitu ambacho waziri alisema sasa hakitakuwepo tena.
Utaratibu huu ulikuwa ukitumika zaidi katika Chuo Kikuu Huria ambapo wanafunzi walikuwa wakisoma programu maalum zilizokuwa zikiwapa sifa ya kusoma Shahada.
“Kilichojitokeza ni kuna taarifa zinasambaa kwamba kuanzia sasa wanafunzi watakaoenda chuo kikuu ni wale ambao tu wamepitia form six sasa hiyo taarifa imeleta presha kubwa, nimekuja hapa sio kukataa tamko hilo hapana nimekuja kulitolea ufafanuzi.” – Naibu Waziri Eng. Stella Manyanya

Raia wa Sudan waendelea kususia shughuli za serikali

- No comments
Raia wa Sudan waendelea kususia shughuli za serikali
















Kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka mashirka mbalimbali nchini Sudan wametoa wito tangu Jumapili Novemba kususia shughuli za serikali kwa muda wa siku tatu mfululizo.
Wito huu ulitolewa kutokana na uamuzi wa serikali wa kuongeza bei ya mafuta, dawa na umeme.Hatua hii ya serikali imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali mahitajio.
Raia wa Sudan wamerusha kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter picha za mitaa tiliyo upu mjini Khartoum na katika sehemu nyingine za nchi hiyo.
Wakati huo huo, maafisa wa usalama wa Sudan, mapema Jumatatu hii asubuhi wamekamata nakala ya magazeti binafsi ya kila siku ya Al-Ayyam na Al-Jareeda bila maelezo.
Kwa mujibu wa magazeti yote mawili, kukamatwa kwa nakala hizo inawezekana kuwa ni adhabu kwa magazeti hayo kutokana na kazi na kuchapishwa kwa habari hiyo kuhusu wito uliyotolewa na wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali kwa raia kususia shughuli za serikali.
Usalama wa Sudan inaweka vikwazo vikali kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na udhibiti kabla ya kuchapishwa habari yoyote.

Fillon ashinda uchaguzi wa mchujo Ufaransa

- No comments
Francois Fillon















Mhafidhina Francois Fillon ameshinda uchaguzi wa mchujo wa chama cha Les Republicains,kwa kutetea sera za kiliberali na "maadili ya Ufaransa". Ushindi huo unampa nafasi nzuri ya kushinda pia uchaguzi wa rais mwakani.

Katika wakati ambapo wafuasi wa mrengo wa kushoto walioko madarakani wanazidi kuzozana,waziri mkuu wa zamani wa Nicolas Sarkozy (2007-2012) anaweza kupambana na mgombea wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia,Front National-FN,Marine Le Pen duru ya pili ya uchaguzi wa rais  itakapoitishwa May 7 mwakani. Na hata kama  Donald Trump amezusha maajabu kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani,taasisi za utafiti wa maoni ya wananchi zinaondowa uwezekano kwa Marine Le Pen kuweza kuingia katika kasri la Elysée.

Mwongozo wake unaotajwa kuwa"mkali" unaonyesha kuwavutia walio wengi."Tunahitaji mageuzi ya kina" alisema Francois Fillon jana usiku akizungukwa na vigogo wote wa kihafidhina. Gazeti la mrengo wa kushoto Liberation,katika toleo lake la leo,linautaja ushindi wa Fillon kuwa ni wenye kuelemea mno upande wa kulia. Kwa mujibu wa mtaalam wa masuala ya kisiasa Jean Yves Camus,mwongozo wa Francolis Fillon utabidi ufanyiwe marekebisho kidogo ikiwa atataka kweli kuwaleta pamoja wafaransa wote na kuepusha mfarakano hasa katika sekta ya mageuzi ya kijamii na kiuchumi.Wafuasi wa siasa za wastani wanataka wapaatiwe ufafanuzi kuhusiana na sera za kijamii pia.
 Francois Fillon atamshinda Marine Le Pen uchaguzi wa rais utakapoitishwa mwakaniChama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front ational kinautaja mwongozo wa Francois Fillon kuwa ni wa enzi za kale.
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi punde,Francois Fillon atampita Marine Le Pen duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais itakapoitishwa April 23 mwakani kwa kujikingia asili mia 26 dhidi ya 24,na kumuacha nyuma kabisa rais Francois Hollande au waziri mkuu wake Manuel Valls,wote wawili wa kutoka chama cha kisoshialisti,ambao wanasemekana watapata asili mia 9 ya kura.
Sera za Francois Fillon kuelekea Urusi na Umoja wa Ulaya zinatia wasi wasi
Mrengo wa kushoto wanamtupia jicho Francois Hollande ambae hadhi na umaaarufu wake unazidi kuporomoka na kukosolewa mpaka na wafuasi wake mwenyewe. Anatarajiwa kutangaza kati kati ya mwezi unaokuja wa decemba kama atagombea mhula wa pili wa miaka mitano,lakini waziri wake mkuu Manuel Valls haondowi uwezekano wa kushindana nae,uchaguzi wa mchujo utakapoitishwa.
Uwezekano wa ushindi wa Francois Fillon katika uchaguzi wa rais wa Ufaransa mwezi May mwakani unazusha baadhi ya hofu nchini Ujerumani na hasa msimamo wake kuelekea Urusi. Na katika masuala ya Ulaya pia,msimamo wa Fillon kuhusu kuundwa serikali ya nchi za kanda ya Euro hauwavutii viongozi wa mjini Berlin.